Alhamisi 8 Oktoba 2026 - 15:00
Damu ya Wanyonge wa Ghaza Imeamsha Dhamiri ya Dunia

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi amesema: Damu ya wanyonge wa Ghaza na kujitolea kwa watu wa Palestina kumeamsha dhamiri ya umma duniani na kuwafanya watu katika nchi mbalimbali kuunga mkono haki za Wapalestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa kutimia miaka mitatu ya vita vya Ghaza, amesisitiza kwamba: Damu ya wanyonge wa Ghaza inaanza kuzaa matunda, na leo suala la Palestina limepata uangalizi katika kiwango cha dunia kuliko wakati mwingine wowote.

Katika ujumbe huo imeelezwa: Damu ya wanyonge wa Ghaza imedhihirisha thamani yake na imegeuka kuwa alama ya nguvu na mwamko. Leo, maoni ya umma duniani yamekuwa makini zaidi kuhusu suala la Palestina, na watu katika maeneo mbalimbali duniani, kwa kulaani hatua zinazochukuliwa na utawala wa Kizayuni, wanadhihirisha mshikamano wao na wananchi wanyonge wa Palestina.

Ameongeza kusema: Hata Umoja wa Mataifa haujaweza tena kunyamaza mbele ya hali hii. Picha za satelaiti za Ghaza zimefichua ukubwa na kina cha uharibifu uliotokea, na ripoti za taasisi za haki za binadamu pamoja na uchunguzi wa Umoja wa Mataifa pia ni ushahidi wa jinai na mateso yaliyowapata wananchi wa Palestina.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, huku akizungumzia jinai zilizotokea Ghaza katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, amesema: Yale yaliyowapata wananchi wa Palestina, hususan wakazi wa Ghaza, katika kipindi hiki, ni miongoni mwa matukio yasiyo na mfano wa mara kwa mara katika ulimwengu wa sasa; lakini ni damu hizi safi na kujitolea kwa wanyonge ndiko ambako leo kumeamsha dhamiri ya umma dunianj na kuufanya umma kuwa makini zaidi kuhusu suala la Palestina.

Ameendelea kusema: Kufanyika maandamano makubwa katika nchi mbalimbali, shughuli za taasisi za haki za binadamu na hatua kama vile “Meli ya Sumud” vinaonesha kwamba uungaji mkono kwa wananchi wa Palestina haujawa na mipaka kwa kundi au mkondo fulani pekee, bali watu kutoka dini, mataifa na matabaka mbalimbali duniani kote wamejitokeza kuunga mkono haki za Wapalestina.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika sehemu nyingine ya ujumbe wake, huku akizungumzia historia ya suala la Palestina, amebainisha: Ardhi ya Palestina imekuwa mhanga wa njama, matamko na makubaliano mbalimbali kwa zaidi ya karne moja. Mchakato huu ulianza kwa Tamko la Balfour mwaka 1917, na tarehe 14 Mei 1948, kwa kuanzishwa utawala wa Israel, ukaingia katika hatua mpya. Baada ya hapo pia, suala la Palestina limepitia hatua mbalimbali kupitia makubaliano na hatua tofauti. Maendeleo na hatua za hivi karibuni pia zinaweza kuchunguzwa katika mwendelezo wa historia hii.

Amesisitiza: Kufanya maamuzi kuhusu mustakabali wa Palestina si haki ya dola au nguvu yoyote ya kigeni; bali ni wananchi wa Palestina wenyewe ambao wanapaswa, kwa kutegemea taasisi, makundi, mikondo inayowawakilisha pamoja na marafiki zao, kufanya maamuzi kuhusu mustakabali wa ardhi yao.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, mwishoni mwa ujumbe wake, akieleza masikitiko na kuwaunga mkono mashahidi wa njia ya kuikomboa Palestina na Baytul-Muqaddas, wakimbizi na wote walioathiriwa na vita, amesisitiza: Uungaji mkono wa kimaadili, kisiasa na kidiplomasia kwa wananchi wa Palestina katika njia ya kufikia haki zao za kisheria, za msingi na halali unapaswa kuendelea.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha